SERIKALI KUTATUA CHANGAMOTO YA MAJI KILOMBERO NA MWANDISHI WETU-MOROGORO. CHANGAMOTO kubwa iliyokuwa ikiwakumba wananchi wa Kilimobero ya uhaba wa maji sasa imepatiwa ufumbuzi wa kudumu baada ya serikali kujenga mradi wa maji katika wilaya hiyo wenye thamani zaidi ya shilingi bilioni 800. Hayo yalisema na Meneja wa Wakala wa Maji Vijijini RUWASA wilaya ya Kilombero

SERIKALI KUTATUA CHANGAMOTO YA MAJI KILOMBERO

NA MWANDISHI WETU-MOROGORO.

CHANGAMOTO kubwa iliyokuwa ikiwakumba wananchi wa Kilimobero ya uhaba wa maji sasa imepatiwa ufumbuzi wa kudumu baada ya serikali kujenga mradi wa maji katika wilaya hiyo wenye thamani zaidi ya shilingi bilioni 800.

Hayo yalisema na Meneja wa Wakala wa Maji Vijijini RUWASA wilaya ya Kilombero Mhandisi Florence Mlelwa ambapo alisema mradi huo utawanufaisha wananchi zaidi ya elifu 20 wanaoishi vijiji 10 vya wilaya hiyo ya Kilombero.

“Kwa ujumla mradi huu unakwenda vizuri na utakapokamilika wananchi wa vijiji 10 katika wilaya hii watanufaika kwa kupata maji safi na salama hali itakayosaidia kuondoa changamoto ya maji maeneo mbalimbali ya wilaya hii”alisema Mlelwa.

Mhandisi Mlelwa alisema kwa muda mrefu wananchi wa Kilombero wamekuwa waikikabiliwa na changamoto ya uhaba wa maji na kwamba serikali imesikia kilio chao na kuamua kutoa fedha kwa lengo la kuhakikisha wananchi wanapata maji.

Alisema mbali na mradi huo pia Wakala wa Maji Vijijini utahakikisha tatizo la maji katika wilaya hiyo linakwisha kabisa na kubaki kuwa historia ambapo aliwata wananchi kuwa na imani na seriali yao kwani changamoto zilizipo zitatatuliwa.

Aidha Mhandisi Mlelwa waliwataka wananchi wote wa vijiji vyote 10 vinavyopitiwa na mradi huo kuhakikisha wanaitunza miundo mbinu ya maji kwani bila hivyo kunaweza kusababisha wakazi wa vijiji hivyo kukosa maji.

Kwa upande wao wananchi na wakazi wa vijiji hivyo wameishukuru serikali kwa kuwakumbuka na kuamua kutatua changamoto ya maji iliyokuwa ikiwakabili kwa muda mrefu ambapo walisema sasa nao wataanza kuona kuwa wanaishi Tanzania.

Lucy Jackson ni miongoni mwa wananchi hao alisema mradi huo utasaidia kumaliza kero ya maji iliyokuwa ikiwakabili hasa wanawake kwani baadhi yao ndoa zilijikuta kwenye migogoro kutokana na kwenda mbali kutafuta maji.

“Wakati wa kiangazi huwa tunatembea zaidi ya kilometa 25 kutafuta maji,tukiwatuma watoto wetu wa kike wazazi tunabaki na mashaka kama watafika na kurudi salama hivyo tunashukuru sana kupata mradi huu”alisema Lucy.

Naye Gabriel Laurent alisema kuwa sasa wananchi wa vijiji hivyo wameanza kuona nuru kutokana na adha iliyokuwa ikiwakabili kutatuliwa ambapo aliahidi kuwa mstari wa mbele katika suala la ulinzi wa miundo mbinu ya mradi huo.

Kwa upande wake Mkuu wa wilaya ya Kilombero Ismail Mlawa amemtaka Meneja wa wakala wa Maji Vijijini wa wilaya hiyo kusimamia kikamilifu miradi hiyo na kwamba kila wakati atapenda kupata taarifa za miradi yote ya maji.

Jfive Team
ADMINISTRATOR
PROFILE

Posts Carousel

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked with *

Latest Posts

Top Authors

Most Commented

Featured Videos

Translate »