Serikali itaendelea kusimamia umoja wa wazanzibari.

Serikali itaendelea kusimamia umoja wa wazanzibari.

Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar inaendelea kusimamia Umoja wa Wazanzibari na kulinda haki za Wananchi wake ili wanufaike na matunda ya Serikali yao. Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Alhajj Hemed Suleiman Abdulla ameeleza hayo wakati akiwasalimia Waumini wa Masjid Safinatu Najaa Mtoni Kidatu alipojumuika nao katika Ibada ya Sala ya Ijumaa. Amesema Serikali

Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar inaendelea kusimamia Umoja wa Wazanzibari na kulinda haki za Wananchi wake ili wanufaike na matunda ya Serikali yao.

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Alhajj Hemed Suleiman Abdulla ameeleza hayo wakati akiwasalimia Waumini wa Masjid Safinatu Najaa Mtoni Kidatu alipojumuika nao katika Ibada ya Sala ya Ijumaa.

Amesema Serikali ya Awamu ya Nane inayoongozwa na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Ahajj Dkt. Hussein Ali Mwinyi inaendelea na ujenzi wa miradi mikubwa ya maendeleo ambapo umoja na mshikamano wa wananchi kwa kushirikiana na Serikali kutapelekea kukamilika kwa miradi hiyo.

Aidha, Alhajj Hemed amewataka Wazazi na Walezi kuwashawishi watoto wao waliokosa nafasi za kujiunga na Kidato cha Tatu kujiendeleza na Masomo katika Vituo vya Mafunzo ya Amali ili kuendelea kupata Wataalamu wa Fani mbali mbali hapo baadae.

Amesema suala la Elimu ni la lazima kwa kila Mtu ambapo Serikali Imejenga Vituo vya Mafunzo ya Amali kwa lengo la kutoa fursa kwa Vijana kujiendeleza na Masomo ya Ufundi ili waweze kujiajiri na kujikimu kimaisha.

Alhajj Hemed amesisitiza Watoto walio chini ya miaka Kumi na Nane wanalazimika kuwa chini ya uwangalilizi wa Wazazi wao hasa katika suala la kusoma jambo ambalo litawaepusha na kujiunga na makundi maovu pamoja na kujiepusha na Vitendo vya udhalilishaji katika jamii.

Sambamba na hayo Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar ameeleza kuwa Serikali inahitaji Watendaji watakaofanya kazi wenye na hofu ya Mungu, waadilifu na wasiojihusisha na Vitendo Vya rushwa na uhujumu Uchumi Nchini.

Akitoa Khutba Mskitini hapo Sheikh Said Mwinyi ameeleza kuwa ni wajibu wa Waumini wa Dini ya Kiislamu kutumia vyema Siku hizi Tukufu kwa kukumbushana Mambo ya kheri yanayomridhia Allah (S.W) ili kupata Radhi zake na kujiandaalia Makaazi mazuri baada ya maisha ya hapa Duniani.

Aidha Sheikh Said ameeleza kuwa miongoni mwa siku bora katika mwezi huu ni siku ya Arafa ambapo ni vyema kwa Waumini kufunga siku hiyo ambapo faida yake ni kufutiwa dhambi za Miaka Miwili.

Imetolewa na Kitengo cha Habari (OMPR)
23 Juni, 2023

Jfive Team
ADMINISTRATOR
PROFILE

Posts Carousel

Latest Posts

Top Authors

Most Commented

Featured Videos

Translate »