WAKALA wa Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi imesaini hati ya makubaliano na Taasisi ya Zanzibar Maisha bora Fondation.

WAKALA wa Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi Zanzobar imetiliana saini hati ya makubaliano na Taasisi ya Zanzibar Maisha bora Fondation (ZMBF) kwa lengo la kushirikiana na kinamama na vijana katika kilimo cha mwani. Hafla ya utiaji saini imefanyika katika ofisini za Taasisi ya Zanzibar maisha bora Foundation Migombani na kushuhudiwa na Katibu Mkuu Ofisi ya Rais, Kazi, Uchumi

WAKALA wa Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi Zanzobar imetiliana saini hati ya makubaliano na Taasisi ya Zanzibar Maisha bora Fondation (ZMBF) kwa lengo la kushirikiana na kinamama na vijana katika kilimo cha mwani.

Hafla ya utiaji saini imefanyika katika ofisini za Taasisi ya Zanzibar maisha bora Foundation Migombani na kushuhudiwa na Katibu Mkuu Ofisi ya Rais, Kazi, Uchumi na Uwezeshaji Maryam Juma Sadala.

Akizungumza mara baada ya utiaji saini huo Katibu Maryam lengo la mashirikiano hayo ni kuyawezesha makundi hayo kukua kiuchumi na kijamii kwani taasisi hiyo ni imara na ipo mstari wa mbele kuhakikisha jamii inakuwa na ustawi mzuri. 

Alisema Zanzibar kuna kundi kubwa la wanawake na vijana ambao wamejikita katika kuzalisha mwani ili kuweza kujipatia kipato na kujikwamua na umasikini.

Aidha aliipongeza ZMBF kwenda sambamba katika dira ya nchi ya uchumi wa buluu hasa kuwasaidia wakulima wa zao hilo kujiajiri na kujipatia kipato.

Katibu Maryam alibainisha kuwa serikali tayari imeshatoa shilingi bilioni 17 kwa wajasiriamali hivyo aliahidi kuwa wizara itahakikisha inasimamia ipasavyo mashirikiano hayo ili makundi hayo yaweze kuinuka kiuchumi na kimaendeleo. 

Hata hivyo, alisisitiza kuandaa mpango kazi wa makubaliano hayo na kuunda kamati ya pamoja itakayosaidia kukutana angalau kila mwezi kwa ajili ya kujadiliana mambo mbalimbali.  

Naye Ofisa Mtendaji Mkuu wa ZMBF, Fatma Fungo, alisema taasisi hiyo imeweza kuwasaidia wanawake wa kilimo cha mwani katika maeneo mabalimbali Unguja na Pemba ndani ya mwaka mmoja ambao wamejikusanya katika vikundi 14 vinavyojishughulisha na kilimo hicho.

Alisema ZMBF imevisaidia vikundi hivyo kuwapatia vifaa mbalimbali ikiwemo boti ziweze kuwarahaisishia kwa ajili ya kulima mwani ambapo jumla ya shilingi milioni 132 zimefikia tangu kupata vikundi hivyo Unguja na Pemba.

Alibainisha kuwa bado kuna nafasi ya kuwawezesha wakulima hao kwani wamekuwa wakitumia mwani huo kutengeneza vitu mbalimbali.

“Sasa tunafajika kuona kwamba bidhaa zao zinaingia katika soko la ushindani na mashirikiano haya yanakwenda kuboresha maisha ya vijana na kina mama katika kuongeza ubora ulio zaidi lengo kuu kuimarisha uchumi wa kina mama na vijana,” alisema.

Naye Mkurugenzi wa Wakala wa Uwezeshaji wananchi Kiuchumi Juma Burhan Mohamed na Mwenyekiti wa Bodi ya wakala huo  Zeena Juma Amour, walisema mashirikiano yanakwenda kuwasaidia vijana na wanawake kwenye sekta nzima ya mwani ambayo ndio ajenda ya serikali kuinua wakulima.

Walimpongeza Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Hussein Ali Mwinyi kwa juhudi zake za kuwasaidia wanawake na vijana kujikomboa katika maisha yao kwani sekta hiyo ni sekta muhimu na inakusanya watu wengi zaidi hivyo ipo haja taasisi hizo kushirikiana ili kuipeleka mbele zaidi. 

Akizungumza kwa niaba ya Mwenyekiti wa Zanzibar Maisha Bora Foundation, Dk. Mohamed Hafidh amempongeza Rais Mwinyi kwa jitihada zake za kuwawezesha wananchi wake kiuchumi na kimaendeleo.

Hata hivyo, alimpongeza Mwenyekiti wa taasisi hiyo Mama Mariam Mwinyi kwa kuuanzisha taasisi hiyo ili iweze kuwasaidia wanawake na vijana namna ya kuwafikisha katika masoko na kuwaomba wanawake na vijana wanaojishughulisha na kilimo hicho kuzitumia fursa hizo.

Jfive Team
ADMINISTRATOR
PROFILE

Posts Carousel

Latest Posts

Top Authors

Most Commented

Featured Videos

Translate »