TRA YAPANDISHA KODI YA MAJENGO

TRA YAPANDISHA KODI YA MAJENGO

Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) kwakushirikiana na Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) imesema Serikali imefanya mabadiliko ya Sheria ya Serikali za Mitaa ya Utozaji wa Kodi ya Majengo, SURA 289 kupitia Sheria ya Fedha ya 2023 ambapo viwango vya utozaji kodi hiyo vimebadilika pamoja na wigo wa ukusanyaji kodi hiyo umeongezeka kwa kujumuisha nyumba zilizopo

Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) kwakushirikiana na Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) imesema Serikali imefanya mabadiliko ya Sheria ya Serikali za Mitaa ya Utozaji wa Kodi ya Majengo, SURA 289 kupitia Sheria ya Fedha ya 2023 ambapo viwango vya utozaji kodi hiyo vimebadilika pamoja na wigo wa ukusanyaji kodi hiyo umeongezeka kwa kujumuisha nyumba zilizopo maeneo yote ya Wilaya.

Viwango hivyo vya utozaji Kodi ya Majengo vilivyobadilika na ambavyo vitaendelea kutozwa kupitia ununuzi wa umeme ni nyumba ya kawaida iliyokuwa inatozwa shilingi 12,000 kwa mwaka sasa itatozwa shilingi 18,000/ kwa mwaka sawa na shilingi 1,500 kwa mwezi.

Nyumba za ghorofa katika maeneo ya Majiji, Manispaa na Halmashauri za Miji zilizokuwa zinatozwa shilingi 60,000 kwa kila sakafu kwa mwaka sasa zitatozwa shilingi 90,000 kwa kila sakafu kwa mwaka sawa na shilingi 7,500 kwa mwezi.

Nyumba za ghorofa katika maeneo ya Halmashauri za Wilaya zilizokuwa zinatozwa shilingi 60,000 kwa kila nyumba kwa mwaka sasa zitatozwa shilingi 90,000 kwa kila nyumba kwa mwaka sawa na shilingi 7,500 kwa mwezi.

Utekelezaji wa kutoza kodi hii ya majengo kwa kufuata mabadiliko tajwa hapo juu, unaanza mwezi Julai, 2023.

Jfive Team
ADMINISTRATOR
PROFILE

Posts Carousel

Latest Posts

Top Authors

Most Commented

Featured Videos

Translate »