SERIKALI IMEWEKEZA FEDHA NYINGI KWENYE SEKTA YA AFYA.

SERIKALI IMEWEKEZA FEDHA NYINGI KWENYE SEKTA YA AFYA.

SERIKALI kupitia Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) na Wizara ya Afya imewekeza fedha nyingi kwenye sekta ya afya ili kuhakikisha hakuna mwananchi atakayekosa huduma bora ya afya. Waziri wa Afya, Mhe. Ummy Mwalimu ameyasema hayo Oktoba 3, 2023 kwenye kongamano la afya lililofunguliwa na Rais wa Serikali ya Mapinduzi

SERIKALI kupitia Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) na Wizara ya Afya imewekeza fedha nyingi kwenye sekta ya afya ili kuhakikisha hakuna mwananchi atakayekosa huduma bora ya afya.

Waziri wa Afya, Mhe. Ummy Mwalimu ameyasema hayo Oktoba 3, 2023 kwenye kongamano la afya lililofunguliwa na Rais wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, Mhe. Dkt.Hussein Mwinyi, jijini Dar es salaam.

“Serikali ya awamu ya sita kupitia Wizara ya Afya na TAMISEMI imewekeza fedha nyingi sana kwenye afya na sasa ni jukumu la kila mmoja kuhakikisha kuwa hakuna mtu anayekosa kupata huduma hiyo,”amesema.

Aidha, amesema itaendelea kuwajengea uwezo watoa huduma za afya ngazi ya msingi kwa kuwa wao ndio wanahudumia wananchi wengi kwa wakati mmoja.

Hata hivyo, amesema serikali inapitia upya mpango wa bima kwa wote ili kujumuisha jamii kubwa ya watumia katika huduma za bima.

Akifungua kongamano hilo, Rais Mwinyi amesema serikali imesema ipo kwenye mpango mkakati wa kuboresha huduma za afya ili kutimiza lengo la kufikia huduma za afya kwa watu wote nchini.

Amesema serikali kuwekeza fedha nyingi kwenye miundombinu ya afya na kwasasa imeweka mikakati ya kuhakikisha huduma zinazotolewa ziwe bora na zimfikie kila mwananchi.

Kongamano la afya linafanyika kwa siku tatu na linawaleta pamoja washiriki Zaidi ya 900 huku mada 34 zikijadiliwa na wataalamu wa sekta ya afya kutoka mataifa mbalimbali.

Jfive Team
ADMINISTRATOR
PROFILE

Posts Carousel

Latest Posts

Top Authors

Most Commented

Featured Videos

Translate »