WATU 92,561 WAMEFIKIWA NA HUDUMA YA AFYA MVOMERO.

WATU 92,561 WAMEFIKIWA NA HUDUMA YA AFYA MVOMERO.

Mkuu wa Wilaya ya Mvomero  Mkoani Morogogoro Mhe. Judith Nguli ametoa wito kwa Wananchi kuwa na desturi ya kupima afya mara kwa mara. Mhe.Nguli amebainisha hayo Turiani Wilayani Mvomero Mkoani Morogoro katika Maadhimisho ya Siku ya Afya Duniani yaliyokwenda sambamba na kaulimbiu isemayo”Afya Yangu Haki Yangu” “Watu wengi wanadhani afya ni kuwa mnene,muonekano mzuri, afya kutoumwa,

Mkuu wa Wilaya ya Mvomero  Mkoani Morogogoro Mhe. Judith Nguli ametoa wito kwa Wananchi kuwa na desturi ya kupima afya mara kwa mara.

Mhe.Nguli amebainisha hayo Turiani Wilayani Mvomero Mkoani Morogoro katika Maadhimisho ya Siku ya Afya Duniani yaliyokwenda sambamba na kaulimbiu isemayo”Afya Yangu Haki Yangu”

“Watu wengi wanadhani afya ni kuwa mnene,muonekano mzuri, afya kutoumwa, lakini si kweli, dhana ya afya ni pana unaweza kuwa mnene ,muonekano mzuri, mtu asifikirie kuwa wewe unaumwa lakini kumbe ndani unaumwa na pale mtu inapofika anaanguka chini pale unaposhuhudia mtu anakata roho ndipo unafikiri huyu kalogwa, katupiwa jini,unampeleka kwa mganga wa Kienyeji kumbe huyo alikuwa na Presha,hakuwa akijijua alikuwa anajiona yuko sawa hivyo ni muhimu tupime afya zetu”amesema.

Akimwakilisha Mkurugenzi Msaidizi Sehemu ya Elimu ya Afya kwa Umma kutoka Wizara ya Afya Dkt. Tumaini Haonga, Simon Nzilibili amesema takkriban Wananchi  wamefikiwa na  huduma mbalimbali za afya .

“Katika maadhimisho haya kwa hapa Mvomero tumefikia zaidi ya wananchi elfu tisini  huduma na huduma zilizokuwa zikitolewa ni pamoja na huduma za chanjo,Ugawaji wa vifaa vya kujipima VVU,Upimaji wa Presha ,huduma za uzazi wa Mpango,huduma rafiki kwa vijana,elimu ya afya kwa Umma,huduma ya uzazi wa Mpango”amesema.

Mratibu wa Maadhimisho hayo Kitaifa Grace Msemwa amesema lengo la maadhimisho hayo ni kuhakikisha jamii inapata elimu kwa usahihi kuhusu masuala mbalimbali ya afya pamoja na huduma za afya.

Nao baadhi ya Wananchi waliopata huduma mbalimbali za afya kupitia Maadhimisho ya Siku ya Afya Duniani  akiwemo Joseph Fungo pamoja na  Elizabeth Severine  wameishukuru Serikali kwa kuadhimisha siku ya afya duniani kwa kutoa huduma bure katika jamii husika Kijijini.

Ikumbukwe kuwa Maadhimisho ya Siku ya Afya Duniani yamekwenda Sambamba na Kaulimbiu isemayo”Afya Yangu,Haki Yangu ambapo kwa hapa nchini pamekuwa na Bonanza la Michezo Turiani Wilayani Mvomero Mkoani Morogoro huku huduma mbalimbali za Afya zikitolewa tangu April 4, 2024 .

Jfive Team
ADMINISTRATOR
PROFILE

Posts Carousel

Latest Posts

Top Authors

Most Commented

Featured Videos

Translate »