Waziri Mkuu akagua athari za mafuriko Taweta, Masagati, Utengule na Malinyi.

Waziri Mkuu akagua athari za mafuriko Taweta, Masagati, Utengule na Malinyi.

WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amewataka wananchi waliokumbwa na adha ya mafuriko nchini waendelee kuwa watulivu wakati Serikali ikiendelea kuratibu utoaji wa misaada kwenye maeneo yaliyoathirika. “Barabara ya Mkongo hadi Utete na ile ya kutoka Mloka Mkongo zote zimeathirika. Tunafanya kazi ya kurejesha mawasiliano ili wananchi waweze kupata huduma muhimu,” amesema. Waziri Mkuu ametoa wito huo

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiwapungia mkono wananchi wa Halmashauri ya Mlimba, Wilaya ya Kilombero Mkoani Morogoro, wakati alikagua athari zilizosababishwa na mafuriko yaliyotokana na mvua kubwa zinazoendelea kunyesha nchini katika maeneo ya Taweta, Masagati, Utengule na Malinyi. Aprili 16.2024.

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na wananchi wa Halmashauri ya Mlimba, Wilaya ya Kilombero Mkoani Morogoro, baada ya kukagua athari zilizosababishwa na mafuriko yaliyotokana na mvua kubwa zinazoendelea kunyesha nchini katika maeneo ya Taweta, Masagati, Utengule na Malinyi. Aprili 16.2024.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na wananchi wa Halmashauri ya Mlimba, Wilaya ya Kilombero Mkoani Morogoro, baada ya kukagua athari zilizosababishwa na mafuriko yaliyotokana na mvua kubwa zinazoendelea kunyesha nchini katika maeneo ya Taweta, Masagati, Utengule na Malinyi. Aprili 16.2024.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na Mkuu wa Mkoa Pwani Abubakar Kunenge, wakati alipowasili wilayani Rufiji, mkoani Pwani kukagua athari za mafuriko kwenye eneo hilo. Hadi sasa waathirika 740 wako kambini. Aprili 16.2024.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na wananchi wa Kata ya Chumbi wilayani Rufiji, mkoani Pwani wakati alipokagua athari za mafuriko kwenye eneo hilo. Aprili 16.2024.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiwapa pole wananchi wa Kata ya Chumbi wilayani Rufiji, mkoani Pwani wakati alipokagua athari za mafuriko kwenye eneo hilo. Hadi sasa waathirika 740 wako kambini. Aprili 16.2024.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiwapa pole wananchi wa Kata ya Chumbi wilayani Rufiji, mkoani Pwani wakati alipokagua athari za mafuriko kwenye eneo hilo. Hadi sasa waathirika 740 wako kambini. Aprili 16.2024.

WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amewataka wananchi waliokumbwa na adha ya mafuriko nchini waendelee kuwa watulivu wakati Serikali ikiendelea kuratibu utoaji wa misaada kwenye maeneo yaliyoathirika.

“Barabara ya Mkongo hadi Utete na ile ya kutoka Mloka Mkongo zote zimeathirika. Tunafanya kazi ya kurejesha mawasiliano ili wananchi waweze kupata huduma muhimu,” amesema.

Waziri Mkuu ametoa wito huo leo jioni (Jumanne, Aprili 16, 2024) wakati akizungumza na wananchi wa kata ya Chumbi, wilayani Rufiji, mkoani Pwani ambako alikwenda kukagua athari za mafuriko kwenye eneo hilo. Hadi sasa waathirika 740 wako kambini.

Waziri Mkuu ambaye aliwasili Ikwiriri, Rufiji akitokea Mlimba, Morogoro aliwaomba  wananchi hao waendelee kutulia kwani serikali iko nao na itaendelea kuwahudumia hadi hali yao irejee katika hali ya kawaida.

“Naomba mpokee salamu za pole kutoka kwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan, tunatambua kuna watu wamepoteza mali na wengine mifugo,” amesema.

Amewataka watendaji wa vijiji waendelee kubaini maeneo mapya ya kuishi ambayo yatatumika kuhamisha kaya zilizoathirika. “Watendaji wa vijiji tuainishe maeneo mapya ya kwenye miinuko ili baadaye watu waweze kuhamishiwa huko,” amesema.

Katika hatua nyingine, Waziri Mkuu ameziagiza TARURA, TANROADS na TAZARA zishirikiane kufanya ukarabati katika maeneo yote yaliyopata athari wakati Serikali inasubiri kumalizika kwa mvua ili iweze kufanya ukarabati mkubwa.

Waziri Mkuu amefuatana na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira), Dkt. Selemani Jaffo, Naibu Waziri wa Nchi (OWM-SBU), Ummy Nderiananga, Msemaji Mkuu wa Serikali, Bw. Mobhare Matinyi na watendaji wengine.

Jfive Team
ADMINISTRATOR
PROFILE

Posts Carousel

Latest Posts

Top Authors

Most Commented

Featured Videos

Translate »